MADAKTARI KUTOKA CUBA WASHUKA HOSPITALI YA MLOGANZILA

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili –Mloganzila imewapokea wataalamu bingwa 10 kutoka nchini Cuba ikiwa ni mikakati yake ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya hususani huduma za kibingwa.  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema wataalamu hao ni wa uuguzi, usingizi, madaktari wa wodi za wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na